full screen background image
5160985_photolol_jpeg40d0559e51ab73fc07961e7bef021b09

KANISA LA KUONDOA PEPO WACHAFU KWA BIA LASHAMIRI KONGO

 

KWA kweli duniani kuna mambo, kumekuweko na makanisa mengi yanaanzishwa kila siku na kila moja viongozi wake wakinadi kuwa wao ndio njia sahihi, kali imeanza huko Kongo, katika jiji la Pointe Noire, kanisa jipya linalojulikana kwa jina la  Louzolo Amour limeanza nalo linahubiri kuwa kunywa bia kunaweza kuondoa mapepo. Kanisa hilo limeanza kupata wafuasi wengi sana. Kanisa hilo lilianzishwa na  Guy Emile Loufoua Cetikouabo, ambaye anadaiwa kuwa yeye ndie Mungu  haonekani kwa macho ila anawakilishwa duniani na kiongozi wa sasa  wa kanisa hilo Charles Mikoungui Loundou. Charles huwaambia wafuasi wake kuwa kiongozi wao  Guy Emile loufoua Cetikouabo alikuwepo, yupo na atakuwepo milele, na kuwa alizaliwa bila kitovu jambo ambalo
linaonyesha Umungu wake.
Kanisa hilo linaamini kuwa kunywa bia kwa imani kunaifanya bia iwe “biéramicine”, kitu ambacho kinaweza kuponya maradhi na kuondoa pepo. Ibada za kanisa hili huchukua hata saa 9, watu wakinywa na kusafisha roho zao.  5160986_k_png129e7547e9b958dbd5e0be43e811fced 5160984_lol2_png1de8d72ac6edf853aca0db0002c9f1ec
 Mmoja wa waumini, Kondi Jean-Jacqyues alisema,’Nilimleta ndugu yangu hapa alikuwa anaumwa na brother Mikoungui alinipa chupa ya bia, nilipokunywa funda tatu nikapandisha mapepo, baada ya hapo nikajisikia niko vizuri sana’. 
Kanisa linawafuasi kama 5000 nchini Kongo. Inasemekana umaarufu wake unaongezeka kwa kasi kiasi serikali haina uwezo wa kulizuia.
Kwenye miaka ya themanini kanisa lililojiita la Mitume wa Mwisho lilianzishwa
Iringa vijijini na kanisa hilo pia lilitumia ulanzi kwa wingi kwa kudai kuwa ni
divai. Na pia lilikuwa likiruhusu wakristu wake kuoa zaidi ya mke mmoja.
Likaanza kuwa maarufu sana Iringa Vijijini.Leave a Reply

Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
%d bloggers like this: