full screen background image
HELL

BADO NINA UCHUNGU MWINGI

Yaliyonikuta jana bado machozi yananitoka. Nilikuwa kituoni nasubiri basi la mwendokasi na abiria wengine. Nilikuwa nimevaa headphone nasikiliza muziki kutoka kwenye simu yangu mpya niliyokuwa nimeishika mkononi, ambayo haina hata wiki. Ghafla likaanza valangati mama mmoja mtu mzima hivi aliyeonekana kuwa ana uwezo wa kifedha, akawa anadai ameibiwa simu. Ghafla akaiona simu yangu nakuanza kudai kuwa ndio simu yake iliyopotea. Nikiwa sina hili walal lile akanizaba kofi la nguvu mpaka nikaona nyota, wananchi wengine nao wakaanza kunizonga na kuniita mwizi na nikaanza kupigwa. Bahati nzuri akatokea polisi na kuingilia kati na kusimamisha adhabu ile kali niliyokuwa napewa. Tukasindikizana na yule mama huku njiani akinitukania wazazi na ndugu zangu wote kuwa wamenifunza wizi. Tulipofika kituoni baada ya maelezo ya pande zote mbili, askari mmoja akamuuliza yule mama namba ya simu yake, na kisha akapiga, simu ikaanza kuita lakini si ile yangu, upande wa pili alipokea binti wa yule mama na kusema simu ni ya mama yake ameisahau nyumbani. Nilianguka kilio zaidi kutokana na maumivu na hata aibu iliyonipata kuitwa mwizi na kupigwa kituo cha basi bila kosa lolote. Yule mama akaniomba msamaha akafungua begi lake na kutoa kitabu cha cheki na kuniandikia cheki ya milioni mbili kuniomba msamaha. Niliondoka kituoni haraka na kuelekea benki, nilipofika nikapanga foleni iliyokuwa ndefu kupata fedha zangu za kifuta jasho na uchungu. Ile nafika tu kwa mhudumu, ghafla nasikia swaiba wangu ananiamsha, ‘Oyaa Kitime amka twende darasani acha uvivu’ Yaani nikikumbuka machozi bado yananitiririka
Leave a Reply

Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
%d bloggers like this: