HATUPIMI BANDO SIE


KUSIKILIZA EFM 93.7 BONYEZA HAPA

EFM
othmmkck

BREAKING NEEEEEWSSS….KUMBE MAREHEMU ALIKUWA MZIMA KABLA HAJAFA

Watu wengi katika mtaa wa Msichoke walionekana wakiwa na huzuni kubwa  nje ya nyumba ya marehemu. Marehemu alikutwa kajinyonga na barua yenye maelezo ilikutwa pembeni ya mwili wake. Marehemu ambaye  alikutwa kajinyonga kutumia kanga ambayo haikuwa ya mkewe, aliacha barua iliyokuwa ina maneno machache sana, askari mmoja aliisoma barua hiyo iliyosema, ‘Tafadhali polisi msimsumbue mtu yoyote, mi mwenyewe nimekufa kwa ridhaa yangu mwenyewe’ Uchunguzi uliofanywa na polisi umegundua mambo mengi yasiyokuwa ya kawaida. Jambo ambalo limewashangaza wachunguzi hao makini ni kuwa marehemu kumbe alikuwa mzima kabisa kabla hajafa. Polisi bado wanapeleleza hili liliwezekanaje. Blog hii makini inaendelea kufuatia hili

Mwandishi wenu.
Leave a Reply

Your email address will not be published.