HATUPIMI BANDO SIE


KUSIKILIZA EFM 93.7 BONYEZA HAPA

EFM
funny_cartoon_dog_riding_bicycle_card-r99f365de9b2f4ccfa455b89ffac2cb01_xvua8_8byvr_324

BREAKING NEWWWS-MBUZI WANGU ATAWATENGENEZEA GARI LENU

Yaani kuna sehemu nyingine ubingwa wake ni kujulikana kwa uchawi, yaani jamaa wanakuwa wachawi mpaka ukiambiwa unatakiwa kwenda huko kikazi haraka sana unaacha kazi. Ila kuna watu wanaamini uchawi mpaka wakisikia kuna sehemu kama hizo ndio kwanza wanaelekea huko kusafisha nyota, kuroga maadui zao , kutafuta vyeo basi tabu tupu.

Jamaa yangu moja mjanja mjanja wa mjini alipata bahati ya kupata fedha kidogo, akawa ana ndoto ya kutumia vizuri hizo fedha ili atajirike. Akapata washauri wakamwambia aende mkoa fulani, siutaji wasije wakaniibukia, huko akaelekezwa atakutana na wataalamu wanaoweza kumtajirisha kwa mtaji aliyokuwa nao. Akatajiwa majina ya matajiri wakubwa waliowahi kupitia huko, jamaa yangu akachanganyikiwa akakodi Noah haraka na kuelekea kwa wataalamu akatajirike.

Safari ilichukua siku moja na nusu, hatimae wakaacha miji na kuingia porini wakifwata maelekezo ya waliokuwa wakiwakuta njiani. Katikati ya pori gari likazimika. Wakajaribu kila njia kufanya hiki na kile gari halikuwaka. Pembeni kidogo kulikuwa na kundi la ng’ombe wako malishoni, japo hapakuonekana mchungaji yoyote. Katika hali ya kukata tamaa mara ng’ombe mmoja akasogelea lile gari, akawasalimia, “Poleni jamani hamjambo?” Jamaa yangu na dreva wake kidogo waingie chini ya gari, mimacho ikawatoka hawaamini kilichotokea, eti ng’ombe kawasalimia. Yule ng’ombe akakohoa kidogo kisha akasema, “Nyie vipi nawasalimia hamnijibu, sio ustaarabu huo, Hamjambo?’ Kwa woga mkubwa jamaa wakajibu,’Hatujambo’. Ng’ombe akawaambia, “Mnajua hilo gari lenu tatizo litakuwa filta ya mafuta, sasa hapo mbele, sio mbali, kuna kijiji, kaulizieni mkipata filta mpya badilisheni gari litakuwa poa’ Baada ya hapo ng’ombe akageuza na kuendelea kula majani. Baada ya sekunde kama nne hivi jamaa akili ziliwarudia walijikuta wakitimua mbio mpaka wakatokea kijiji cha jirani. Wakaanguka kwa uchovu wananchi wakawazunguka, mzee mmoja akawauliza ‘Vipi jamani?’ Jibu lao wakihema kwa nguvu lilikuwa “Ng’ombe, ng’ombe”. Wakaulizwa “Ng’ombe kafanya nini?”.Majibu yao “Mzee gari letu liliharibika akaja ng’ombe katuambia eti filta mbovu”. Yule mzee kawauliza, ‘Mhh ng’ombe mwenyewe alikuwa rangi gani?” ‘Mweusi anabaka jeupe kichwani’. Duh wanakijiji wote wakaguna na kuanza kutawanyika, yule mzee ndie akacheka kabisaa. ‘Hahahaha yule ng’ombe mweusi tunamjua wote hapa kijijini mwongo sana yule, hebu ngoja sindikizaneni na mbuzi wangu, akawachekie hilo gari lenu, maana mbuzi wangu ndie anaejua mambo ya ufundi wa magari” Jamaa zangu wakazimia
Leave a Reply

Your email address will not be published.