HATUPIMI BANDO SIE


KUSIKILIZA EFM 93.7 BONYEZA HAPA

EFM
hell_forever_and_ever

ILE ILIKUWA KAMPENI TU

KATIKA  mizunguko yake huku na kule kwa bahati mbaya mwanasiasa mmoja maarufu akagongwa na gari akafa. Alipofika kwenye lango la mbinguni akakuta mlinzi wa lile lango, akamakaribisha, “Karibu karibu huku ndio mbinguni, ila unanichanganya kidogo umefikaje huku maana wanasiasa kuja huku ni mara chache sana ngoja niulizie tukuweke wapi”. Yule mwanasiasa akajitetea akasema ,’Bwanae mimi nataka kuishi huku mbinguni, maana mimi ndie nilikuwa mkombozi wa wananchi wangu’. Baada ya mawasiliano na ngazi za juu yule mlinzi wa geti la mbinguni akamwambia mwanasiasa, ‘Nimepewa maelekezo kuwa wewe utembelee masaa 24 motoni na masaa 24 hapa mbinguni kisha uchague utakaa wapi, maana nyie wanasiasa huwa hamchelewi kuanza kuchanganya watu’

Basi akaingizwa kwenye lifti na kushushwa motoni. Kufika kule akakuta mambo tofauti na mawazo yake, kawakuta wanasiasa wenzie kibao wana majengo ya kifahari, usafiri wa kifahari kuliko walivyokuwa duniani, kila mmoja ana mke mzuri wakakumbatiana na kuanza kukumbushana mambo mengi ya zamani, wakazunguka sehemu mbalimbali watu wote walikuwa wanaonekana wanafuraha, jioni ile alitayarishiwa hafla ya chakula cha hali ya juu na hotuba zikatolewa kumkaribisha na kumwambia hayo ndio maisha ayategememee. Baada ya hapo akaenda kulazwa hoteli kubwa na kuaahidiwa nyumba kubwa mara atakapohamia rasmi. Hata ndoto usiku ule zilikuwa tamu sana.

Kesho yake akapandishwa juu mbinguni, kwanza akakuta watu wote hawafahamu, na muda mwingi walikuwa wakiruka ruka kwa mabawa yao toka wingu moja mpaka jingine wakisali na kumsifu Mungu kwa furaha waliyonayo. Baada ya masaa 24 kuisha mbinguni mwanasiasa alirudishwa getini, na akaambiwa umeshaonja pande zote mbili, sasa jibu utakalotoa halitabadilishwa milele unataka kwenda wapi? Bila kusita akaanza,’Kwa kweli  sikutegemea kama ntajibu swali hili hivi, ukweli ni kuwa nataka kwenda motoni’ Basi lifti ikafunguliwa akaingia na kuteremka kwenda motoni.

Kufika kule kakuta mambo tofauti na jana yake. Kulikuwa na joto kali, giza harufu mbaya, mazingira mambovu ,rafiki zake ambao jana yake walionekana matajiri wenye furaha walikuwa wamejikunyata wachovu wanalia kwa maumivu yasiyoeleweka na watu wote wako hali mbaya kuliko maelezo. Shetani akamwambia ‘Karibu Jehanamu’. Mwanasiasa akaonyesha mshangao mkubwa na kuuliza, ‘Mbona sielewi, jana nimekuja hapa palikuwa pazuri sana na niliahidiwa kila kitu kitakuwa hivi milele, sasa imekuwaje?’ Shetani akacheka aksema, ‘ Acha hizo mwanasiasa, unakuwa kama hujui mambo ya siasa? Jana tulikuwa tunapiga kampeni, sasa si umeshapiga kura, hii ndio hali halisi’

 
Leave a Reply

Your email address will not be published.