ISIMILA FESTIVAL


KUSIKILIZA EFM 93.7 BONYEZA HAPA

EFM
IMG_20170417_170700

MKUU WA WILAYA YA IRINGA AWAJIA JUU WAHARIBIFU WA UOTO ASILI

Wananchi mjini Iringa wakiendelea kufyeka miti kuandaa maeneo ya biasharaNa Fredy Mgunda, Iringa


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwachukulia hatua watu wote waliohusika na uharibifu wa mlima uliopo Kata ya Kitanzini Miyomboni kutokana na mlima huo kuwa ni hifadhi ya taifa.
Kasesela alisema kuwa amesikitishwa na wananchi walivamia mlima huo na kuanza kujenga vibanda wakati kuna maeneo mengi yapo hapa Manispaa hivyo ni lazima hatua zichukuliwe ili kutunza uoto wa asili.

“Nimefika katika eneo lile kweli wananchi wamevamia, nafikiri wametumia fursa ya sikukuu hii ya Pasaka kufanya uharibifu huo, na sitakubali kuona kukiukwa kwa maagizo ya Makamu wa Rais kuhusu kutunza uoto wetu wa asili” alisema Kasesela

Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kulifiatilia swala hilo na kuhakikisha vibanda vyote vilivyojengwa viwe vimevunjwa na kuanza kupandwa miti maeneo yote yaliyokatwa miti na kuhakikisha eneo liloharibiwa linarudi kwenye ubora wake.

“Kufikia kesho saa nne vibanda vitakuwa vimebomolewa hatuwezi kuaharibu eneo kama lile lazima wachukuliwe hatua kuanzia wananchi hadi viongozi waliohusika na mpango huo kwa kuwa wananchi hawawezi kuanza wenyewe bila kupata ruhusa kutoka kwa viongozi fulani” alisema  Kasesela

Lakini Kasesela alisema kuwa atakikisha anawachukulia hatua viongozi wenye uelewa mdogo wa namna ile kwa sababu kiongozi mwenye akili na uelewa mkubwa hawezi kuruhusu kuaharibiwa eneo hilo.

Nawaomba wananchi wa Manispaa ya Iringa na Wilaya yote ya Iringa kuwa makini wanapoambiwa kufanya biashara katika mazingira yaliyohifadhiwa kwa kuwa wanaharibu mazingira makusudi na pia wanapata hasara zisizo kuwa na maana mfano walivamia huo mlima tayari wameshapata hasara lakini wameipa hasara kubwa serikali na jamii yote.


Uharibifu mkubwa unaofanywa katika mlima huo ukifumbiwa macho kama ilivyo ni wazi uongozi wa Manispaa ya Iringa utakuwa umepuuza agizo la makamu wa Rais na uwezekano wa uhifadhi wa ikolojia ya mto Ruaha kwa mwendo huo itakuwa ni ndoto ya alinachaLeave a Reply

Your email address will not be published.