HATUPIMI BANDO SIE


KUSIKILIZA EFM 93.7 BONYEZA HAPA

EFM
giphy

RAIS TRUMP AMFUTA KAZI BOSI WA FBI NA KUANZISHA ZOGO JINGINE MAREKANI

 

James Comey
Donald
Trump kamfukuza kazi Mkurugenzi wa FBI James Comey, taarifa kutoka White House zinasema kuwa Mkurugenzi huyu amefukuzwa kutokana na ushauri wa Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions.
Katika barua ya kufukuzwa kazi ambayo James Comey ameandikiwa na Rais wake, moja ya sababu ambazo zimefanya afukuzwe ilikuwa ni… “not able to effectively
lead”  na kuwa FBI inahitaji uongozi mpya ili kuaminika zaidi. Itakumbukwa kuwa Mkurugenzi huyu pia alilalamikiwa na Democrats kuwa alitoa taarifa zilizosababisha Mama Clinton kunyimwa kura. James Comey amekiri kuwa taarifa alizozitoa kuhusu emails za siri  hazikuwa sahihi. Zogo kubwa limeshaanza kutokana na kufukuzwa huku kwani Democrats wanahoji kwanini Comey afukuzwa sasa wakati alikuwa akiongoza uchunguzi dhidi ya tuhuma kuwa Warusi walimuwezesha Trump kushinda. Kitendo hicho kimefananishwa na kile cha Rais Nixon kumfukuza kazi mkuu wa FBI wakati akiwa katika uchunguzi wa tuhuma ya Watergate iliyomuondoa Rais huyo madarakani. Picha linaanza utamu.

Rais mpya wa Korea Kusini na mkewe

Jambo jingine jipya ni kuwa Korea Kusini imepata Rais mpya anaitwa Moon Jae-in, na tayari amekwisha sema angependelea kuwa na mazungumzo na kiongozi wa Korea kaskazini, jambo ambalo ni wazi halitaifurahisha Marekani.
Leave a Reply

Your email address will not be published.