full screen background image

SAMAHANI NATAFUTA ANAEWEZA

Jamaa alikuwa anaumwa akapita kituo cha taxi akaikuta taxi moja, akamuomba sana taxi dreva ampeleke hospitaji lakini fedha yake ilikuwa ndogo, kitu cha ajabu dreva alimporomoshea jamaa matusi ya nguoni na kumwambia akapande bodaboda kama hana hela.

Wiki mbili baadae jamaa akawa amepona na anapesa mkononi, akaenda kituo cha taxi akakuta taxi nne ikiwemo ya yule dreva aliyewahi kumtukana, akamwendea dereva wa kwanza;

JAMAA: Natafuta dereva wa taxi shoga niondoke nae ntamlipa laki

DEREVA 1: We mwenda wazimu nini hebu toka hapa.. Jamaa akenda taxi ya pili

JAMAA: Samahani Bradha natafuta dereva shoga niondoke nae ntamlipa laki

DEREVA 2: Pumbavu mkubwa, hizi bangi mnazovuta zinawaletea uchizi, unaniona mie shoga? toka hapa

Hatimae jamaa akaenda kwa yule taxi dreva aliyewahi kumtukana

JAMAA: Aise sijui unaweza kunipeleka Ubungo?

DEREVA: Ndio shilingi alfu kumi

JAMAA: Haya twende….wakati wanaondoka jamaa akahakikisha anapungia mkono wale madereva waliobaki kituoni huku akionyesha alama ya kidole gumba. Akiwaacha midomo wazi
3 thoughts on “SAMAHANI NATAFUTA ANAEWEZA

Leave a Reply

Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
%d bloggers like this: