full screen background image
timthumb

UNATAKA KUJIUNGA NA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)?

 

timthumb

TaSUBa inawatangazia umma nafasi za kujiunga na kozi kwa ngazi ya Cheti (Certificate) na

Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2015 /2016

 

Kozi hizo ni kama ifuatavyo:-

 1. Sanaa za Maonyesho (Performing Arts):-

Muziki, Ngoma, Tamthiliya/Maigizo, Sarakasi na Sanaa za Ufundi

 1. Ubunifu na Uzalishaji wa Muziki (Music Design and Production)
 2. Picha Jongefu (Media Design and Film Production)

– Masomo ya sayansi ya Jamii, ICT, Kiswahili na Kiingereza yatafundishwa kwa wote.

– Mwombaji kozi namba mbili (2) na namba tatu (3) awe na ujuzi wa kompyuta.

 

NGAZI YA CHETI KWA MIAKA MIWILI

Sifa za Kujiunga

– Aliyemaliza Darasa la Saba (Standard Seven) na ambaye hakuhitimu kidato cha Nne

– Aliyehitimu kidato cha Nne na hakufanikiwa kupata wastani wa “D” nne (4)

ANGALIZO:

– Ngazi hii ni kwa Masomo ya Sanaa za Maonyesho TU.

– Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM B

 

NGAZI YA CHETI KWA MWAKA MMOJA

Sifa za Kujiunga

– Aliyemaliza kidato cha nne na kupata wastani wa “D” nne (4)

ANGALIZO:

– Watakaofaulu wastani wa ‘B’ baada ya kuhitimu ngazi ya cheti wataruhusiwa kujiunga

na Stashahada (Diploma) kwa miaka miwili.

– Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A

 

NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA)

Sifa za Kujiunga

– Awe amefaulu kidato cha sita na kupata principal pass 1 na subsidiary 1

– Awe amehitimu ngazi ya cheti cha sanaa za maonyesho na ufundi kwenye chuo kinachotambuliwa na NACTE

ANGALIZO:

 • Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A

MAELEZO MENGINE

– FOMU za kujiunga zinapatikana Chuoni pia kwenye tovuti ya chuo www.tasuba.ac.tz

– Kila mwombaji atalipia ada ya FOMU ya Tsh.15,000/=kupitia NMB BANK akaunti

Na. 2101100012 yenye jina UTAWALA CHUO CHA SANAA

– Maombi yaambatanishwe na stakabadhi ya malipo (Receipt/Bank Pay Slip) ya Tsh.

15,000 kwa ajili ya FOMU.

– Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31/05/2015 na maombi yote yatumwe kwa; MTENDAJI MKUU, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania.

– Kwa MAELEZO zaidi wasiliana nasi kupitia namba za simu: 0715974100, 0763408792, na 0715394933 au Barua pepe [email protected]

 
15 thoughts on “UNATAKA KUJIUNGA NA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)?

 1. meshack charles bruno

  naomba nipewe form no A niko mkoani na ninahitaji kujiunga na music design and production
  natanguliza shukran zang za dhati kwenu

  Reply
 2. john james

  jamani nataka kusomea music design and music production, but fomu za kujiunga na chuo sizioni mtandaooni! zinazoonekana ni za 2015/2016, 2016/2017 hazioneksni. nisaidieni

  Reply

Leave a Reply

Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com
%d bloggers like this: